- angalia
- kujifunza
- mazoezi
-
Habari gani, unataka msaada?
Nchini China ukienda benkini kutoa malipo ya matumizi ya umeme au maji nyumbani, huenda mhudumu anaweza kukuuliza: 您好, 要帮忙吗?
您好 nín hǎo, habari gani.
要 yào, taka.
帮忙 bāng máng, toa msaada.
吗 ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Nataka kutoa malipo ya matumizi ya simu.
我 wǒ, mimi.
交 jiāo, toa.
电话 diàn huà, simu.
费 fèi, gharama, malipo.
-
Habari gani, unataka msaada?
-
Ndiyo, nataka kutoa malipo ya matumizi ya simu.
-
Tafadhali nifuate.
-
Asante.
-
Usijali.