Nchini China benki zinaonesha umuhimu wake katika maisha ya watu, mbali ya kuweka akiba, watu pia wanaweza kwenda benkini kutoa malipo ya matumizi ya simu, gharama za matumizi ya internet, kununua umeme wa matumizi ya nyumbani, kuomba mikopo, kubadilisha fedha za kigeni na kadhalika. Kama saa 1 asubuhi utaona msururu mbele ya benki, hakika watu hao wengi wanasubiri kununua dhamana za taifa, kwani kununua dhamana hizo watapata faida zaidi kuliko kuweka akiba benkini.
Hivi sasa mabenki makubwa mbalimbali yamechukua hatua za aina mbalimbali za kutoa huduma bora kwa ajili ya wateja, huduma za benki na ufanisi wake umeboreshwa zaidi kuliko zamani.