-
Rafiki yako akikohoa sana, unaweza kumwambia: 你得去看医生。Ni lazima uende kuonana na daktari.
你 nǐ, wewe.
得 děi, ni lazima.
去 qù, enda.
看 kàn, ona.
医生 yī shēng, daktari.
-
Wakati unataka rafiki yako kukufuata kwenda hospitali unaweza kusema: 你能陪我去医院吗? Unaweza kufuatana nami kwenda hospitali?
你 nǐ, wewe
能 néng, weza.
陪我 péi wǒ, kufuatana nami.
去 qù, enda.
医院 yī yuàn, hospitali.
吗 ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Kabla ya kuonana na daktari, unatakiwa kupata namba moja ya kusubiri kwanza. Unaweza kuwauliza watu wengine: 在哪儿挂号?Niende wapi kupata namba moja ya kusubiri?
在哪儿 zài nǎr, wapi.
挂号 guà hào, kupata namba ya kusubiri.
-
Ukitaka kuonana na mtaalamu hospitalini, unaweza kusema: 挂一个专家号。Nataka kupata namba ya kusubiri kukutana na mtaalamu.
挂 guà, pata.
一个 yí gè, moja.
专家 zhuān jiā, mtalaamu.
号 hào, namba.