somo 45 Kupata namba ya kusubiri hospitalini

 ongea na CRI
 

Katika miji mbalimbali pamoja na miji midogo ya wilaya nchini China, kuna hospitali zenye ukubwa tofauti, na baadhi ya idara za serikali au mitaa pia kuna zahanati ndogo. Kwa kawaida, watu wakipata ugonjwa kwanza wanaweza kwenda kwenye zahanati zilizo karibu nao. Kama wakienda hospitali, wanatakiwa kusubiri kwa muda, hasa wakitaka kukutana na madaktari wataalamu, wanatakiwa kwenda hospitali asubuhi mapema, halafu wanasubiri kwa muda mrefu, kwani wataalamu ni wachache, ambao kila siku wanaweza kukutana na wagonjwa wachache tu. Hivi sasa hospitali kubwa mbalimbali zimeanzisha huduma zao kwenye tovuti zao katika mtandao wa internet kwa ajili ya kuwasaidia watu kuagiza siku ya kukutana na madaktari wataalamu.