Katika elimu ya matibabu ya kichina, wagonjwa wanapotibiwa pia wanaweza kushughulikia hali ya miili yao, kuongeza uwezo wa kinga, kwa kufanya hivyo hawawezi kupata madhara makubwa, hivyo wagonjwa wengi waliopatwa na ugonjwa sugu, au wazee na watoto wanapotibiwa, huwa wanaweza kuchagua kwanza matibabu ya kichina. Katika maduka ya dawa za mitishamba ya kichina, kuna dawa za aina mbalimbali, wahudumu wanaweza kuwasaidia wateja kupata dawa walizoandikiwa na madaktari, ambapo wateja pia wanaweza kuwaambia wahudumu hali yao ya ugonjwa, ili wawasaidie kupata dawa zinazowafaa.