- angalia
- kujifunza
- mazoezi
-
Unaweza kunisaidia?
Wakati tunaponunua vitu kwenye maduka, kwenda benkini, au kula chakula kwenye mikahawa, huwa tunahitaji misaada ya wengine. Tunaweza kusema, "Tafadhali unaweza kunisaidia?" kwa Kiswahili. Na kwa Kichina ni "nǐ néng bāng wǒ yī gè máng mā?" "nǐ": wewe; "néng": kuweza; "bāng wǒ": nisaidie; "bāng": kusaidia; "wǒ": mimi; "yī gè": moja; "máng": msaada."mā" ni kisaidizi cha neno kwa kuuliza kama "je" kwa Kiswahili. "bāng máng" , maana yake ni kusaidia."bāng wǒ yī gè máng" yaani kunisaidia. "nǐ néng bāng wǒ yī gè máng mā?": Unaweza kunisaidia?
-
Hakika naweza.
Kama mwingine aliyeombwa akiweza, anaweza kusema bila shaka, kwa Kichina ni “dang ran ke yi”. “dang ran”, hakika; “ke yi”, weza.