Uhusiano kati ya majirani ni muhimu katika jumuia ya kichina. Kama mume na mke wakigombana vikali, majirani huja kuwaonya mpaka wapate maafikiano. Mume na mke wote wakiwa na kazi, wanaweza kumpa jirani ufunguo wa nyumba, na kumwomba yeye amtunze mtoto wake aliyerudi toka shuleni. Lakini, hivi sasa watu wengi wanaishi katika nyumba zenye ghorofa, na majirani hawafahamiana. Wakazi wengi hata wazee wanaona uhusiano baina ya watu siyo mzuri kama zamani. Hali kadhalika, majirani wanaanza kuwasiliana kwa kutumia njia mpya, kama vile mtandao wa internet.