somo 5 omba msaada

 ongea na CRI
 

  • Unaweza kunisaidia?
    Wakati tunaponunua vitu kwenye maduka, kwenda benkini, au kula chakula kwenye mikahawa, huwa tunahitaji misaada ya wengine. Tunaweza kusema, "Tafadhali unaweza kunisaidia?" kwa Kiswahili. Na kwa Kichina ni "nǐ néng bāng wǒ yī gè máng mā?" "nǐ": wewe; "néng": kuweza; "bāng wǒ": nisaidie; "bāng": kusaidia; "wǒ": mimi; "yī gè": moja; "máng": msaada."mā" ni kisaidizi cha neno kwa kuuliza kama "je" kwa Kiswahili. "bāng máng" , maana yake ni kusaidia."bāng wǒ yī gè máng" yaani kunisaidia. "nǐ néng bāng wǒ yī gè máng mā?": Unaweza kunisaidia?

  • Hakika naweza.
    Kama mwingine aliyeombwa akiweza, anaweza kusema bila shaka, kwa Kichina ni “dang ran ke yi”. “dang ran”, hakika; “ke yi”, weza.

  • Unaweza kunisaidia kupiga picha?
    Wakati unapotembelea peke yako kwenye bustani, kama unataka mchina mwingine anakusaidia kupiga picha, unaweza kusema: "néng bāng wǒ zhào zhāng xiàng mā?" Tafadhali unaweza kunisaidia kupiga picha? "néng": kuweza; "bāng": kusaidia; "wǒ": mimi; "zhào xiàng": kupiga picha.

  • Nikusaidie nini?
    Wakati fulani watu wanahitaji misaada ya wengine. Kwa Kiswahili "Nikusaidie nini?", kwa Kichina "wǒ néng bāng zhù nǐ mā?" "wǒ": mimi; "néng": kuweza; "bāng zhù": kusaidia; "nǐ" : wewe; "mā" ni kisaidizi cha neno kwa kuuliza.