- angalia
- kujifunza
- mazoezi
-
Nchini China wazazi wa watoto wengi hutaka kuwatafutia watoto wao shule nzuri na wanaweza kupiga simu ya shule moja moja na kuuliza: 您好,请问你们学校有没有班车?Hujambo, tafadhali niambie kuna basi la kuwachukua watoto kwenye shule yenu?
有 yǒu, kuna.
没有 méi yǒu, hakuna.
班车 bān chē, basi la kuwachukua watoto.
-
Kila siku basi hili linawachukua watoto saa ngapi?
每天 měi tiān, kila siku.
几点 jǐ diǎn, saa ngapi.
接 jiē, kupokea.
送 sòng, kupeleka.
-
Hujambo, tafadhali niambie kuna basi la kuwachukua watoto kwenye shule yenu?
-
Shule yetu ina basi la kuwachukua watoto.
-
Kila siku basi hili linawachukua watoto saa ngapi?
-
Basi linawachukua watoto saa 2 asubuhi na kuwarudisha nyumba saa 11 jioni.