Nchini China watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi miaka sita hupelekwa kwenye shule za chekechea. Kwenye shule za chekechea, watoto wanacheza zaidi, pia wanajifunza kazi rahisi kama vile kuchora picha, kutengeneza sanaa rahisi za mikono, na kusoma vitabu vyenye picha. Katika zama za hivi leo, wazazi wa watoto wengi wana matumaini kuwa watoto hao watajifunza mengi ili wawe na mwanzo mzuri wa ukuaji. Ndiyo maana shule za chekechea zinazotoa mafunzo ya kupiga vinanda au kujifunza lugha za kigeni hukaribishwa zaidi.