Katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China, madarasa ya masomo mbalimbali huwa na tofauti kubwa, kwa mfano darasa moja la kujiufnza lugha ya kigeni huwa na wanafunzi zaidi ya 10 tu, ili kila mwanafunzi apate nafasi ya kutosha kufanya mazoezi. Lakini katika madarasa ya masomo kadha wa kadha ya lazima ambayo mafunzo yao yanawafurahisha, kila darasa hujaa wanafunzi wengi hadi kufikia mia kadhaa. Zamani kwenye madarasa ya vyuo vikuu, wanafunzi walisikiliza tu mihadhara ya walimu, lakini hivi sasa wanafunzi wanapenda kujishirikisha katika mafunzo ya darasani, kwa mfano, wanafunzi wanaweza kufanya maonesho darasani, na walimu pia wanapenda kuwashirikisha wanafunzi kufanya majadiliano darasani, ili wanafunzi waelewe na kupata ujuzi vizuri, pia kupata uwezo wa kuchambua na kutatua masuala wao wenyewe, na kupata uwezo wa kufanya uratibu na ushirikiano kati ya vikundi na vikundi.