Kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita, “utamaduni wa baa” ulianza kuonekana zaidi na kimyakimya katika miji mikubwa nchini China, ambapo kustawi kwa uwepo wa baa kulihusiana na ustawi wa uchumi, jamii na utamaduni wa China nzima, katika miji mikubwa nchini China kama vile Beijing, Shanghai na Shenzhen, shughuli za baa ziliendelezwa katika hali motomoto, ambapo kwenye baa za aina mbalimbali mjini Beijing, vinywaji na pombe ni vya aina nyingi, baa za mjini Shanghai ni zenye mvuto wa kipekee wa kuwafurahisha watu, na baa za mjini Shenzhen huonesha hali motomoto, baa kwenye miji mikubwa zimekuwa mahali pa kupumzika na kujiburudisha kwa vijana.