somo 63 Kutazama maonesho ya opera ya Beijing

 ongea na CRI
 

Opera ya Kibeijing ni mchezo wa sanaa wenye sifa nzuri ya taifa la China, opera hiyo imekuwa na historia ndefu, ambayo inaonesha utamaduni mkubwa wa China. Katika michezo ya sanaa ya zaidi ya aina 300 nchini China, opera ya Kibeijing ni mchezo wa sanaa ulioenea kwenye sehemu nyingi zaidi na yenye taathira kubwa zaidi. Kuna wahusika wa aina nne kwenye opera ya Kibeijing, yaani vijana wa kiume na wa kike, wazee na wacheshi kwa jumla. Na kila mhusika ana sura yake pekee, mapambo ya sura hizo yanaonekana kwa rangi tofauti ili kuonesha tabia tofauti.