-
Ukitaka kujua kama unaruhusiwa kupiga picha au la, unaweza kuuliza: 这儿可以拍照吗?Naruhusiwa kupiga picha hapa?
这儿 zhèr, hapa.
可以 kě yǐ, ruhusiwa.
拍照 pāi zhào, piga picha.
吗 ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Usitumie mwanga wa kamera.
请 qǐng, tafadhali.
不要使用 bú yào shǐ yòng, usitumie.
闪光灯 shǎn guāng dēng, mwanga wa kamera.
-
Katika jumba la makumbusha, ukitaka kusikiliza maelezo ya mwelekezaji, unaweza kuuliza: 有解说员吗?Kuna mwelezaji?
有 yǒu, kuna.
解说员 jiě shuō yuán, mwelekezaji.
-
Hivi karibuni kutakuwa na maonesho gani mapya?
最近 zuì jìn , hivi karibuni.
还 hái, tena.
有 yǒu, kuwa na.
什么 shén me, gani.
新 xīn, mapya.
展览 zhǎn lǎn, maonesho.