Nchini China kuna majumba ya makumbusho ya zaidi ya aina 2300. Tangu mwanaelimu maalum wa China Bw. Zhang Qian aanzishe Jumba la kwanza makumbusho la wachina la Nantong, mchakato wa maendeleo ya majumba ya makumbusho ya China umeendelezwa kwa miaka mia moja. Hivi sasa mjini Beijing tu kuna majumba ya makumbusho ya aina mbalimbali yapatayo zaidi ya 140, idadi hii inachukua nafasi ya kwanza duniani. Kuanzia mwaka 2008, majumba 33 ya makumbusho ya mjini Beijing yalifunguliwa kwa watu bila kiingilio.