• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bara la Afrika lataka kutegemea "njia mpya ya hariri" ili kujikwamua kiuchumi chini ya msukosuko wa fedha

    (GMT+08:00) 2009-06-12 18:56:50

    "Njia ya hariri ya kale" ilikuwa njia muhimu ya biashara kati ya Bara la Ulaya na Asia. Tarehe 11 Juni, kongamano kuhusu "kutafiti njia hariri ya China" lilifanyika huko Cape town, Afrika ya kusini, ambapo wafanyabiashara wa zama za kale hawakuwahi kupita nchi hiyo katika biashara zao kwenye "njia ya hariri." Wanasiasa na wafanyabiashara walioshiriki kwenye kongamano hilo walichukua njia ya kuimarisha biashara kati yao na China na kuiga uzoefu wa maendeleo ya China ni kama kutafiti "njia mpya ya hariri", na kutaka kutegemea nji hiyo kuifanya Afrika ijikwamue kiuchumi chini ya msukosuko wa fedha duniani.

    Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa kongamano hilo alisema, njia ya kujiendeleza ya China inatofautiana na ile ya nchi za magharibi, ambayo inastahili kuigwa na Bara la Afrika. Waziri wa maendeleo ya uchumi wa Afrika ya kusini Bw. Ebrahim Petel anaona kuwa, hatua za serikali ya China za kutunga sera zinasitahiki kuigwa na nchi za Afrika. Alisema:

    "Kundi la uchumi la Asia ya mashariki ya China, hasa China, nguvu zao bora zinaonekana kwenye hatua zao za kutupia macho siku za mbele, kutunga mpango kabla ya wakati, na kutoa maamuzi katika hali ambayo haziwezi kupata ufanisi au faida katika kipindi cha muda mfupi; aidha zinaweza kutunga sera za uchumi zenye umuhimu wa kimkakati; na katika wakati wa kuendeleza shughuli zao za uchumi ziwe za aina mbalimbali, zinaweza kuweka mkazo katika kazi za ujenzi wa miundo mbinu, na kuonesha umuhimu wa serikali katika kuendeleza mawasiliano na mawasiliano ya simu. Na wakati wa kufanya ushirikiano na kampuni za nchi za nje, kampuni za China pia zinatilia maanani sana maendeleo yake zenyewe, hivyo tumeona baadhi ya kampuni kubwa za kimataifa zilizopata mafanikio zimejitokeza nchini China katika miaka ya hivi karibuni."

    Kongamano hilo ni moja kati ya shughuli za Mkutano wa 19 wa Afrika wa Baraza la uchumi wa dunia, kongamano hilo linalenga kupata mwangaza kutoka kwa uzoefu wa kujiendeleza wa China. Mwanakampuni wa Nigeria Bw. Busty Okundaye ambaye hivi sasa yuko Shanghai, China kwa kuendeleza shughuli zake, alisema:

    "Serikali za nchi za Afrika ni lazima zichukue hatua halisi, kwa mfano kuanzisha kituo cha utamaduni wa China, ili kuwawezesha watu wajifunze utamaduni wa China, halafu kujenga uwezo wao wenyewe, kujitahidi kujipatia fursa mbalimbali kwa kuinua uwezo wa kiteknolojia na uwezo wa usimamizi."

    Katika mchakato wa kuimarisha mawasiliano kati ya Bara la Afrika na Bara la Asia, wanakampuni wa China wenye busara wametupia macho mapema soko kubwa la Afrika. Mkurugenzi mkuu wa Benki ya viwanda na biashara ya China Bw. Jiang Jianqing alisema:

    "Tumewekeza barani Afrika kwa sababu tumeona soko la Afrika ni zuri sana. Hivyo naona kama Afrika inaweza kushika fursa mbalimbali na kushikilia kufungulia mlango, kurekebishana na kukamilisha hatua kwa hatua mundo wao wa uchumi, hakika Afrika itapata nguvu kubwa zaidi ya kujiendeleza."

    Mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Guijin alisisitiza kwenye kongamano hilo kuwa, serikali ya China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika katika kushinda pamoja matatizo. Alisema:

    "Msukosuko wa fedha duniani umeleta athari Fulani mbaya kwa bara la Afrika, serikali ya China imetoa ahadi yake kwa makini, hatutapunguza misaada kwa maendeleo ya Afrika, bali tutaongeza kwa kiasi cha kufaa. Aidha tutahamasisha kampuni za China ziwekeze zaidi barani Afrika, ili kushirikiana na nchi za Afrika katika kushinda taabu, na kulifanya ongezeko la uchumi na jamii lidumishe mwelekeo mzuri."

    Bw. Liu Guijin alisema, serikali ya China inapenda nchi za Afrika zinufaike na uzoefu na maarifa ya China kuhusu kujiendeleza, kuondokana na umaskini na kuendeleza mambo ya vijiji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako