Leo tarehe mosi Julai ni mwaka wa 99 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambacho ni chama kikubwa zaidi cha kisiasa duniani. Chama hicho ambacho wanachama wake wameongezeka kutoka zaidi ya 50 hadi zaidi ya milioni 90 kimetawala China kwa miaka 71.
Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika mwezi uliopita, viashiria vikuu vya uchumi wa China vimeboreka kwa mfululizo, na uchumi wa China umeendelea kufufuka.
Mikutano mikuu miwili ya kisiasa nchini China ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na Mkutano wa Bunge la Umma la China inayoendelea kufanyika, inafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, ambayo inasema mikutano hiyo itaimarisha imani ya dunia.