• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Hatimaye walioshambulia Westgate Nairobi washindwa

    (GMT+08:00) 2013-09-25 16:10:40

    Rais wa kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba magaidi ambao walikuwa wameshika watu mateka katika jumba la Westgate mjini Nairobi hatimaye wameshindwa na jeshi la nchi hiyo.

    Wakati wa oparesheni ya siku tatu zaidi ya watu 67 waliuwawa wakiwemo pia wanajeshi waliokuwa wakipambana na magadi hao wa alshabab.

    "Tumewaaibisha na kuwashinda maadui wetu"

    Ujumbe huu wa Rais uhuru Kenyatta umekuwa afueni kwa wakenya baada ya siku tatu za makabiliano kati ya polisi na magadi wa alshabab katika jumba la westgate hapa mjini Nairobi.

    Magaidi hao walishambulia na kutwaa jumba hilo jumamosi na hivyo kupelekea maafisa wa polisi kuanza oparesheni kali kuwaokoa mateka waliokuwemo.

    Na mwishoni mwa oparesheni hiyo Rais Uhuru Kenyatta kwenye taarifa kupitia televisheni ya Taifa alitangaza Kushindwa kwa wapiganaji hao wa Al-shabaab .

    "magaidi watano waliuwawa kwa kupigwa risasi. Washukiwa kumi na moja wamezuiliwa kwa kushukiwa kuhusuka na shambilizi hili. Lazima washtakiwe kuambatana na sheria pamoja na wafuasi wao popote walipo"

    Lakini huku oparesheni ya uokoaji ikimalizika bado kuna kazi nyingi iliosalia.

    Kuta tatu za jumba la Westgate zimeanguka na miili kadhaa bado imekwama kwenye vifusi.

    "mwishoni mwa oparesheni hii kuta tatu za jumba la westgate zilianguka nab ado kunayo miili kadhaa bado imekwama katika vifusi ikiwepo pia ya magaidi waliuwawa"

    Zaidi ya watu 60 walipoteza maisha yao wakati wa mamshambulizi haya ambayo ni mabaya kuwahi kutokea kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi.

    Baadhi ya familia zimeweza kutambua miili ya wapendwa wao lakini kwa wengine kama Alfred Musyoki bado hawajapata jamaa zao.

    "Tumekuwa tukimtafuta tangu jumamosi na bado hatujamuona. Tumeenda kwenye meza ya shirika la msalaba mwekundu na hatujafanikiwa. Jina lake ni Anne Mbinya Mutua na alikuwa anafanya kazi kama mhudumu wa nyumbani karibu na Westgate"

    Rais Uhuru Kenyatta ametangaza pia siku tatu za kuomboleza waanga wa mashambulizi haya.

    Wakati wa maombolezi hayo bedera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti kama heshima kwa wlaiopoteza maisha yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako