Klabu ya soka KMKM ya Zanzibar imepata pigo kubwa la kuondokewa na kipa wake Ali Suleiman Bishoo. Kipa huyo ambaye alikuwa namba 1 alifariki kwa kuangukiwa na mti wa aina ya mvinje kutokana na upepo mkali uliovuma. Ajali hiyo ilimkuta akiwa anaendesha vespa wakati alipokuwa akitoka kwenye safari zake za kawaida, maeneo ya mwanakwerekwe wilaya ya mjini Magharibi Unguja. Bishoo alikuwa ni miongoni mwa kipa waliochaguliwa katika timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, lakini alizuiwa na KMKM hivyo kufungiwa kutocheza soka kwa msimu mzima wa ligi za ZFA Taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |