• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli kuanza kujengwa

    (GMT+08:00) 2015-09-01 19:35:19

    Mipango ya ujenzi wa reli ya kisasa itakayowezesha treni kusafiri kwa kilometa 120 kwa saa na kubeba tani milioni 25 kwa mwaka itaanza mwaka huu.

    Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania,, Samuel Sitta amesema miradimengine ya reli za kusafirisha abiria kutoka Daresalaam imeanza kujengwa na Rais Jakaya Kikwete .

    Mradi huo ulishaanza maandalizi yake na sasa utawekewa jiwe la msingi na Rais Kikwete Septemba 15, mwaka huu, hafla itakayofanyika eneo la Soga Mpiji wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

    Kuhusu mradi huo, alisema baada ya Rais kuweka jiwe na msingi, ujenzi wa reli hiyo utafanywa na Kampuni ya China Railway Construction kwa miaka minne na nusu kwa gharama ya Sh trilioni 16.

    Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa pia utaanza kabla ya Rais Kikwete kuondoka madarakani na itaanzia Mtwara hadi katika Bandari ya Mbamba Bay ili kusafirisha rasilimali za chuma, makaa ya mawe na gesi, akisema hatua hiyo itakuza uchumi wa wananchi wa kusini ndani ya miaka minne ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako