Ripoti iliyotolewa na kikundi cha utafiti cha Chuo kikuu cha Imperial cha Uingereza imesema, kuanzia mwaka 2012 hadi 2014, idadi ya watumaji wa sigara ya kielektroniki iliongezeka kutoka asilimia 7.2 hadi asilimia 11.6.
Ripoti hiyo iliyotolewa katikia jarida la "Usimamizi wa Tumbaku" la Uingereza imesema, kikundi hicho kilikusanya takwimu za watu elfu 53 katika nchi 27 za Ulaya na kuzichambua. Kiwango cha watumiaji wa sigara ya kielektroniki cha Ufaransa ni juu zaidi barani Ulaya, ambacho kilifikia asilimia 21.3.
Sigara ya kielektroniki inatengenezwa kwa betri, kifaa cha kupasha moto na maji yenye nikotini. Hivi sasa hakuna thibitisho lolote kuwa sigara hiyo inaweza kusaidia kuacha uvutaji wa sigara, kwa kuwa wavutaji wa sigara wakitaka kuacha tabia hiyo, wanatakiwa kukwepa kabisa nikotini.
Watafiti wanaona kuwa, hivi sasa hawawezi kutabiri matatizo ya kiafya yatakayotokana na sigara ya kielektroniki katika miaka 10 hadi 20 ijayo, na utafiti mwingi zaidi unatakiwa kufanywa kuhusu jambo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |