Matokeo ya utafiti mpya yaliyotolewa katika jarida la taasisi ya matibabu ya Marekani yameonesha kuwa, mazoezi yanaweza kupunguza hatari za aina 13 za saratani, ikiwemo saratani ya ini, saratani ya figo na saratani ya matiti.
Katika utafiti huo, taasisi ya saratani ya taifa ya Marekani imechambua hali za watu milioni 1.44 wa nchi za Ulaya na Marekani, ambao walifuatiliwa kwa miaka 11. Kila wiki walifanya mazoezi ya kukimbia, kutembea na kuogelea kwa dakika 150 ambayo ni sawa na muda wa mazoezi unaopendekezwa na Shirika la Afya la Marekani. Katika kipindi cha utafiti, watu laki 1.87 walipata saratani.
Utafiti huo umechambua aina 26 za saratani, na matokeo yameonesha kuwa kwa kulinganishwa na watu wanaofanya mazoezi kidogo, kwa watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara hatari ya aina 13 za saratani ilipungua kwa asilimia zaidi ya 20, ambayo ni pamoja na saratani ya ini, mapafu, figo na damu.
Jambo lingine linalotakiwa kuzingatiwa ni kwamba, kati ya aina hizo 13 za saratani zinazoweza kupunguziwa hatari kwa mazoezi, aina 10 hazina uhusiano wowote na kupunguza unene. Hii inamaanisha kuwa mfumo wa mazoezi kupunguza hatari ya saratani unaweza kutokuwa na uhusiano na kupunguza uzito.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |