Akiongea kwenye mkutano wa kilele wa miundombinu mjini Nairobi, Macharia amesema, mradi huo uliogharimu dola za Marekani bilioni 3.6 ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 88, umeshachangia asilimia 2 ya ukuaji wa pato la taifa la nchi hiyo GDP.
Macharia ameongeza kuwa, zaidi ya Wakenya 27,000 wameajiriwa chini ya mradi huo, huku miji ambayo reli hiyo inapita ikinufaika kwa kustawi biashara zao. Mbali na hayo amesema mradi huo umeongeza ufanisi wa Bandari ya Mombasa kwa kuwa unahakikisha mizigo inasafirishwa haraka kuliko njia ya usafiri wa barabara.
Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Exim ya China unatarajiwa kukamilika mwakani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |