• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wanajaribu kufichua jeni za kukinga ukame za nafaka ya quinoa ili kuboresha uzalishaji wa nafaka barani Afrika

    (GMT+08:00) 2016-08-10 15:53:33

    Idara mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Kyotona kituo cha utafiti wa kilimo, misitu na uvuvi cha Japan zimetangaza ramani ya jeni za quinoa. Quinoa imesifiwa kuwa mama wa nafaka na watu wa Amerika ya Kusini, kwa sababu inaweza kuishi katika mazingira yenye ukame na ina lishe nyingi. Kutafiti jeni za quinoa kunasaidia kuboresha sifa ya nafaka nyingine.

    Utafiti wa mwanzo unaonesha kuwa quinoa ina jeni zaidi ya elfu 60 zinazoamua tabia mbalimbali. Baadhi ya jeni zinahusiana na uwezo wa kukinga ukame na lishe nyingi.

    Kikundi cha utafiti kitaendelea kutafiti jeni hizi zinafanya kazi gani na jinsi jeni hizi zinazofanya kazi. Watafiti wamesema utafiti huo utasaidia kukuza mazao yenye uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na mazingira magumu, kuboresha jeni za mpunga na ngano, na kuboresha uzalishaji wa nafaka na kutatua tatizo la utapiamlo.

    Quinoa ni nafaka ya kienyeji ya milima ya Andes ya Amerika Kusini, na ni chakula muhimu cha wenyeji wa kabila la Wainka. Ili kuihimiza dunia itambue umuhimu wa nafaka hiyo katika kutatua ukosefu wa nafaka na kuondoa umaskini, Umoja wa Mataifa ulitangaza mwaka 2013 ni mwaka wa quinoa wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako