Watu wengi hawana tabia ya kucheza kamari. Wanapendelea kupata shilingi 1000, moja kwa moja kuliko kucheza kamari ambayo kuna uwezekano wa asilimia 50 tu wa kushinda shilingi 2000. Wanasayansi wamegundua kuwa katika jambo hili mbwa wanafanana binadamu, lakini mbwa mwitu ni tofauti.
Watafiti kutoka kituo cha sayansi ya mbwa mwitu cha Ernstbrunn, Austria wametafiti tabia ya kucheza kamari ya mbwa mwitu 7 na mbwa 7. Walifunika mabakuli mawili juu ya meza. Chini ya bakuli la kwanza kuna chakula kisicho na ladha nzuri, na chini ya la pili kuna nyama tamu au jiwe, uwezekano wa kupata nyama au jiwe ni nusu kwa nusu. Mbwa na mbwa mwitu wote wanajua jambo hili, wanaweza kuchagua kwa kugusa bakuli moja. Katika asilimia 80 ya majaribio, mbwa mwitu walichagua bakuli la pili ili kushinda nyama tamu, lakini katika asilimia 58 ya majaribio mbwa walichagua bakuli la pili.
Watafiti walisema katika miaka elfu 18 hadi 32 iliyopita, binadamu walianza kufuga mbwa, mbwa hawana haja tena ya kuwinda na walikuwa na tahadhari zaidi. Lakini mbwa mwitu wanaendelea maisha ya kuwinda. Wanyama wasiokuwa na uhakika na chakula chao wanapenda zaidi kucheza kamari, sokwe mtu wanaowinda kima na kula matunda katika baadhi ya majira pia wana tabia ya kucheza kamari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |