5. Mbali na habari za kusikitisha lakini wiki hii pia ilipokea habari za faraja kutoka nchini Afghanistan baada ya Serikali ya nchi hiyo na chama cha Hizb-e-Islami kusaini makubaliano ya amani huko Kabul, ili kuhimiza mchakato wa amani na maafikiano ya kitaifa nchini humo. Hayo ni makubaliano ya kwanza kusaniwa na serikali ya Afghanistan na kundi la upinzani lenye silaha tangu mwaka 2001 utawala wa Taliban ulipoondolewa.
Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, kiongozi wa ujumbe wa chama hicho Bw. Amin Karim amesema makubaliano hayo ni "hatua ya kwanza kuelekea kutimiza amani na usalama wa kudumu nchini kote," Ameyataka makundi mengine ya kijeshi yanayopambana na serikali kujiunga na mchakato wa amani. Hata hivyo, Bw. Karim amesisitiza kuwa chama cha Hizb-e-Islami kitaendelea na jitihada zake hadi majeshi ya kigeni yatakapoondolewa nchini Afghanistan.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |