Shirika la kimataifa la mkakati wa kuzuia maafa ya asili la Umoja wa Mataifa UNISDR limetoa ripoti likisema katika miaka 20 iliyopita watu milioni 1.35 wamefariki katika maafa ya asili, miongoni mwao asilimia 56 walifariki katika matetemeko ya ardhi na tsunami.
Ripoti hiyo iitwayo Maskini na Vifo: Idadi ya watu waliofariki katika maafa ya asili kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2015 inasema idadi ya watu waliofariki katika maafa hayo inahusiana moja kwa moja na mapato na kiwango cha maendeleo. Idadi ya watu waliofariki katika nchi zenye mapato madogo na ya wastani katika miaka 20 iliyopita ilikuwa milioni 1.22, ambayo ilichukua asilimia 90 ya watu wote.
Haiti ni nchi inayosumbuliwa zaidi na maafa ya asili yakiwemo matetemeko ya ardhi, ukame na vimbunga, ambako watu laki 2.3 walifariki. Indonesia ina watu laki 1.82 waliofariki, Myanmar ina laki 1.39, China ina laki 1.23 na India ina elfu 97.
Mkurugenzi wa UNISDR ambaye pia ni mjumbe maalum wa kazi ya kuzuia maafa wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Robert Glasser alisema ingawa matetemeko ya ardhi na tsunami yanasababisha vifo vingi zaidi, lakini katika miaka 15 iliyopita, hali ya hewa mbaya imesababisha vifo vyingi zaidi kuliko matetemeko ya ardhi na tsunami, na vifo vingi vilitokea katika nchi zenye mapato madogo na ya wastani ambazo zinatoa hewa chache inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |