• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini kotmiri inapendwa na baadhi ya watu na kuchukiwa na wengine?

    (GMT+08:00) 2016-10-28 09:29:05

    Kotmiri ni mmoja kati ya mimea ya kundi la Apiaceae. Asili ya mboga hii ni katika eneo la bahari ya Mediterrean, ambako pia ni asili ya mboga nyingine za kundi la Apiaceae zenye harufu kali. Jina la kilatin la kotmiri ni Coriandrum sativum, neno la Coriandrum linatoka na neno "koris" katika lugha ya kigiriki cha kale, ambalo linamaanisha mdudu mwenye harufu mbaya. Hii inamaanisha kuwa katika maelfu ya miaka, watu wametambua harufu maalum ya mboga hiyo. Watu wanaoipenda wanaona inanukia, lakini watu wanaoichukia wanasema ina harufu mbaya inayofanana na sabuni au mdudu.

    Harufu ya kotmiri inatokana na kemikali aina ya aldehydes, ikiwemo kemikali ya trans-2-Decenal, ambazo zinafanana na kemikali zilizoko katika majimaji yanayotolewa na baadhi ya wadudu.

    Protini za kunusa harufu za watu mbalimbali zinatofautiana kutokana na jeni tofauti, hivyo watu huwa na maoni tofauti kuhusu harufu moja, kwa mfano, baadhi ya watu wanapenda kunusa harufu ya siki, baadhi wanapenda harufu ya pombe, na baadhi wanapenda harufu ya petroli. Wanasayansi wamegundua kuwa jeni kadhaa ikiwemo jeni aina ya OR6A2 inaamua maoni ya watu kuhusu kotmiri. Watu wenye jeni hizi wanaweza kuhisi harufu ya kemikali aina ya aldehydes kwa urahisi zaidi kuliko wengine, hivyo ni jeni zimewafanya kuchukia kotmiri tangu wazaliwe.

    Watu kutoka sehemu mbalimbali wana maoni tofauti kuhusu kotmiri. Asilimia 21 ya watu wa Asia mashariki wanaichukia, asilimia 17 ya wazungu wanaichukia, na asilimia 7 ya watu wa Asia kusini wanaichukia, lakini asilimia 97 ya watu wa Mashariki ya Kati wanaipenda sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako