Tetemko la ardhi lenye ukubwa wa 6.5 kwa kipimo cha Richter lilitokea tarehe 30 Oktoba nchini Italia, kabla ya hapo, tarehe 26 matetemko ya ardhi yenye ukubwa wa 5.4 na 5.9 yalitokea ndani ya saa 3, na tarehe 24 mwezi Agosti, Italia ilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0. Kwanini hivi karibuni matetemeko mengi ya ardhi yalitokea nchini humo?
Mtaalamu wa taasisi ya fizikia ya dunia na volkeno ya Italia Bw. Warner Marzocchi alisema matetemeko hayo yote yalitokea katika milima ya Appennino, umbali kati ya vitovu vya matetemeko hayo hauzidi kilomita 20. Tetemeko la ardhi la kwanza lililotokea Agosti lilivunja uwiano kati ya mabamba ya ardhi katika eneo hili. Mabamba mbalimbali yanashinikizana, na wakati shinikizo linapokuwa kubwa kupita kiasi, mipasuko mipya inatokea.
Milima ya Appennino ni eneo lenye matetemeko mengi ya ardhi. Kutokana na mwendo wa gamba la dunia, vipande vya Afrika vinakaribia vipande vya Ulaya, na kusababisha matetemeko ya ardhi kutokea katika kanda ya bahari ya Mediterranean.
Mtaalamu huyu anaona kuwa katika wiki au miezi kadhaa ijayo, matetemeko mengi zaidi yatatokea, lakini ukubwa utapungua kidogo kidogo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |