Watu wengi wanaamini kwamba mayai na vifaranga vya ndege vikiguswa na binadamu hata kwa mara moja, watakuwa na harufu ya binadamu, na kutelekezwa na wazazi wao. Lakini maoni hayo hayaendani na hali halisi.
Mwenyekiti wa zamani wa shirika la Marekani la wataalamu wa ndege Bw. Frank B. Gill amesema ingawa ni rahisi kwa ndege kushitushwa, lakini hawawatelekezi ovyo watoto wao, wakiwemo wale walioguswa na binadamu. Ameongeza kuwa ndege wakisumbuliwa wanapojenga viota au wanapotaga, basi huenda wakaacha viota vyao na kujenga vipya katika mahali pengine.
Watu wengi wanadhani ndege wanaweza kuhisi harufu ya binadamu, lakini ukweli ni kwamba ndege hawana uwezo mkubwa wa kuhisi harufu.
Hata hivyo, si vizuri kwa sisi binadamu kurandaranda karibu na viota vya ndege ili tuepushe kuwashitua ndege kwa sababu ndege bado wana uwezekano wa kuwatelekeza watoto wao. Ndege wazazi wanaamua kuwaacha au kutowaacha kwa kufikiria faida na hasara kwanza. Kama wazazi wametumia muda mrefu na juhudi nyingi kuwalisha watoto wao, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba watajaribu kuwapeleka watoto wao kwenye viota vipya badala ya kuwacha moja kwa moja. Aidha, ndege wenye umri mrefu wakiwemo vipanga wanachukia zaidi kusumbuliwa, na wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuwaacha watoto wao kuliko wale wenye umri mfupi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |