Shirika la jiofizikia la Marekani limetoa ripoti mpya likisema katika miongo kadhaa ijayo, matumizi ya maji ya binadamu huenda yakasababisha maji yaliyoko chini ya ardhi kwisha huko India, Ulaya na baadhi ya sehemu nchini Marekani.
Mtalaamu wa maji wa Chuo cha Madini cha Colorado cha Marekani Bibi Inge de Graaf alipotoa hotuba kwenye mkutano wa mwaka wa shirika hilo alisema ifikapo miaka ya 50 karne hii kutokana na matumizi kupita kiasi ya maji yaliyoko chini ya ardhi, watu bilioni 1.8 duniani wataishi katika maeneo yasiyo na maji yaliyoko chini ya ardhi.
Bibi Graaf alisema India, Ulaya na baadhi ya sehemu nchini Marekani zitakabiliwa na hali mbaya zaidi. Hali nchini China itakuwa nzuri kidogo, na sehemu ya kusini mwa China ni nzuri zaidi kuliko kaskazini.
Kabla ya hapo, Shirika la Anga ya Juu la Marekani NASA na idara nyingine zimetafiti maji yaliyoko chini ya ardhi duniani kupitia data zilizokusanywa na satilaiti, na kugundua kuwa kiasi cha maji kinapungua kwa kasi ya kushangaza katika matabaka kadhaa makubwa yenye udongo na mawe yenye mashimo mengi ambayo yanafaa kuhifadhi maji duniani. Bibi Graaf na watafiti wengine wamekadiria muda wa kuisha kwa maji yaliyoko chini ya ardhi kwa mujibu wa data hizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |