Katika mwaka 2012 hadi mwaka 2015, watafiti wa Chuo Kikuu cha Osaka cha Japan waliunganisha protini zinazotoa nuru za viumbe vya baharini vikiwemo sea pansy na yavuyavu, na kuzalisha protini mpya inayoweza kutoa nuru bila kuwekwa chini ya mwanga wa UV, na kuipa jina la "Nano-lanterns".
Hivi karibuni watafiti wa chuo hiki wametoa ripoti katika gazeti la Nature Communications wakisema wameboresha protini ya "Nano-lanterns" kwa kuongeza protini ya kamba wanaoishi katika bahari yenye kina kirefu. Sasa protini hiyo inaweza kutoa nuru yenye rangi 5, na kiwango cha nuru kimeinuliwa kwa mara 2 hadi 10.
Watafiti wakitumia protini mpya, wamefanikiwa kuchunguza miundo mitano midogomidogo ndani ya seli, pia wamechunguza kwa mara ya kwanza mchakato wa kuundwa na kuvunjika kwa molekuli ya protini. Wamesema protini inayotoa nuru za rangi mbalimbali itarahisisha uchunguzi wa seli za viumbe.
Katika miaka 60 karne iliyopita, wanasayansi waligundua kwa bahati protini inayotoa nuru ya rangi ya kijani chini ya mwanga wa UV mwilini mwa yavuyavu. Wanasayansi walirekebisha protini hiyo na kuifanya itoe nuru ya rangi nyingine, na baadaye walizalisha protini inayotoa nuru bila ya mwanga wa UV. Mwaka 2008 wanasayansi watatu waliogundua protini inayotoa nuru walipewa tuzo ya kemikali ya Nobel.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |