• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duma wako hatarini duniani

    (GMT+08:00) 2016-12-29 09:43:59

    Watafiti kutoka shirika la wanyama la London, shirika la uhifadhi wa wanyama pori wa familia ya paka la Panthera na shirika la uhifadhi wa wanyama pori nchini Uingereza wamefanya utafiti na kutoa ripoti kwenye gazeti jipya la Proceedings of the National Academy of Sciences la Marekani, wakitoa onyo kwamba idadi ya duma ambao ni wanyama wanaokimbia kwa kasi zaidi duniani ni 7100 tu, wako katika hatari ya kutoweka.

    Watafiti wamesema licha ya kupungua kwa idadi ya duma, maeneo wanakoishi pia yamepungua kuwa asilimia 9 tu ya maeneo ya zamani. Duma wanaoishi barani Asia wanaathiriwa zaidi, hivi sasa idadi ya duma wanaoishi nchini Iran ni chini ya 50. Idadi ya duma wanaoishi nchini Zimbabwe imepungua kuwa 170 kutoka 1200 katika miaka 16 iliyopita.

    Watafiti wamesema kupotea kwa maskani, ukosefu wa chakula unaosababishwa na uwindaji kupita kiasi wa wanyama wengine, uwindaji haramu na biashara ya duma vimetishi maisha ya duma. Aidha, asilimia 77 ya duma wanaishi nje ya hifadhi mbalimbali, hivyo ni rahisi zaidi kuathiriwa na vitendo vya binadamu.

    Kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya duma, watafiti wametoa wito kulitaka shirika la uhifadhi wa maumbile la kimataifa kuweka duma kwenye orodha ya wanyama walioko hatarini badala ya wanyama walioko katika hali ngumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako