Teknolojia ya VR ambayo inawawezesha watu kuona picha au video za 3D ni moja kati ya teknolojia za kisasa zinazofuatiliwa na watu wengi. Lakini wakati vyombo hivi vinavyotumiwa na watu wengi zaidi wakiwemo vijana na watoto, suala jipya linatakiwa kutiliwa maani. Je, vyombo hivi ni salama kwa watoto ambao ubongo na macho yao bado hayajapevuka?
Makampuni ya Samsung na Oculus yanasema watumaji wa vyombo vya VR wanatakiwa kufikia umri wa miaka 13, kampuni ya Sony inawataka watumaji wafikie umri wa miaka 12, na makampuni ya HTC na Google yanapendekeza watoto wasitumie vyombo hivi au kuvitumia chini ya usimamizi wa wazima.
Baadhi ya watu wanahisi kizunguzungu wanapotumia vyombo vya VR, hili ni tatizo kubwa la vyombo hivi. Vyombo vya VR vinaonesha picha mbili zinazopigwa katika pande tofauti kwa macho mawili ili kuwafanya watu wahisi picha za 3D. Tofauti na hali ya kutazama vitu halisi, watu wanaopotumia vyombo vya VR, macho yao yanaaangalia zaidi umbali mmoja, lakini vitu vinavyooneshwa kwenye picha vinaonekana viko katika umbali tofauti. Hali hii inafanya ubongo wa binadamu uchanganywe, na kusababisha watu kuhisi kizunguzungu.
Mwaka 2014, watafiti wa Marekani waligundua kuwa panya wakitazama picha au video za 3D, zaidi ya nusu ya neva zinapumzika. Hali hii inakuwa ni tofauti kabisa na wakati wanapotazama vitu halisi. Dr. Michael Madary wa Chuo Kikuu cha Mainz cha Ujerumani alisema utafiti kuhusu athari ya VR kwa binadamu bado haujaanza kufanywa, lakini wazazi wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa na wasifanye majaribio kwa watoto wao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |