Hivi karibuni Uholanzi yenye vituo vyingi vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya upepo imepiga hatua nyingine kubwa katika matumizi ya nishati safi. Kuanzia tarehe 1 Januari, treni zote za umeme nchini humo zinatumia umeme uliozalishwa kwa nguvu ya upepo.
Msemaji wa kampuni ya reli ya Uholanzi amefamisha kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya kampuni yake na kampuni ya nishati ya Eneco yalipanga kutimiza lengo mwaka 2018, lakini kutokana na juhudi kubwa, lengo hili limetimia mwaka huu.
Kampuni ya reli ya Uholanzi inaendesha treni 5,500 kwa siku, miongoni mwa treni hizi, treni za umeme zina uwezo wa kusafirisha abiria laki 6 kwa siku. Uholanzi umetangulia duniani katika matumizi ya nishati ya upepo kwenye reli.
Umeme unaozalishwa kwa saa moja na mtambo wa kawaida wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya upepo unaiwezesha treni kusafiri kilomita 190. Kampuni ya reli ya Uholanzi na kampuni ya Eneco zinapanga kuboresha teknolojia husika, ili kupunguza matumizi ya umeme kwa asilimia 35 ifikapo mwaka 2020 ikilinganishwa na mwaka 2005.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |