Kampuni ya Ushauri ya "Mageuzi" ya Uingereza imetoa ripoti ikikadiria kuwa, kutokana na maendeleo ya teknolojia ya akili bandia, katika siku zijazo roboti huenda zitachukua nafasi laki 2.5 za ajira katika sekta ya huduma za umma, kupunguza gharama ya uendeshaji na kuinua ufanisi wa kazi.
Ripoti hiyo imejadili suala la nguvu kazi katika idara za serikali, matibabu, elimu na usalama wa umma, na kusema ifikapo mwaka 2030, roboti itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi badala ya watumishi wa serikali laki 1.3 wa hivi sasa, na kupunguza gharama ya pauni bilioni 2.6 kwa mwaka.
Katika sekta ya matibabu, teknolojia mpya pia itatumiwa badala ya wafanyakazi laki 1.14 wanaofanya kazi za kiutawala na kupokea wagonjwa, na kupunguza gharama ya pauni bilioni 1.7. Kazi za wauguzi na madaktari pia huenda zitaathiriwa, kwani programu za kompyuta zimepata mafanikio katika upimaji wa baadhi ya magonjwa, na matumizi ya roboti za upasuaji pia yameongezeka.
Mmoja kati ya waandishi wa ripoti hiyo ambaye ni mtafiti mwandamizi wa kampuni ya "Mageuzi" Bw. Alexander Hitchcock anasema, kueneza matumizi ya roboti ili zifanye kazi badala binadamu ni suala nyeti linalotakiwa kushughulikiwa kwa makini, lakini teknolojia mpya itazifanya huduma za umma ziwe nzuri zaidi, zenye usalama zaidi na za bei nafuu zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |