• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jinsi wafugaji wa Ujerumani wanavyoshughulikia kinyesi

    (GMT+08:00) 2017-03-01 15:30:00

    Ujerumani ni nchi inayozalisha na kula nyama nyingi ya nguruwe. Mwaka jana idadi ya nguruwe wanaofugwa nchini humo ilikuwa milioni 27. Lakini kinyesi cha nguruwe hakikusababisha uchafuzi wa mazingira. Wakulima wa huko wanashughulikia vipi kinyesi? Mwandishi wa habari ametembelea shamba la kufuga nguruwe huko Brandenburg.

    Kiongozi wa shamba hili Bw. Florian Schultz alisema kinyesi cha nguruwe kinaingia kwenye mabomba yaliyoko chini ya sakafu, mwishowe kuingia kwenye tangi. Kitatumiwa kama mbolea au kuzalisha umeme.

    Licha ya kufuga nguruwe, kampuni yake pia inafuga ng'ombe, kulima mazao mbalimbali yakiwemo ngano nyekundu, shayiri na ngano. Kinyesi cha ng'ombe ambacho kinakauka zaidi kinafaa kutumika katika kuzalisha gesi ya kinyesi halafu kuzalisha umeme, na kile cha nguruwe kinafaa zaidi kuzalisha mbolea.

    Kwa mujibu wa kanuni za mbolea zinazotekelezwa nchini Ujerumani, muda na matumizi ya mbolea za kinyesi yanatakiwa kudhibitiwa kwa makini ili kuzuia matumizi kupita kiasi ya mbolea kuathiri mazingira, hasa kuchafua maji. Katika majira ya baridi, mbolea hizi zinapigwa marufuku kutumiwa, na mahitaji ya umeme ni makubwa, hivyo vinyesi vya nguruwe na ng'ombe vyote vinatumiwa kuzalisha umeme.

    Kampuni ya kuzalisha umeme kwa kinyesi iko kilomita 8 kutoka shamba hili. Kiongozi wa kampuni hii Bw. Fred Schultz alisema kampuni hii inaweza kuzalisha umeme kilowati 546 kwa siku, kujenga kampuni hii ili kuzuia kinyesi cha mifugo kisichafue mazingira ni uamuzi mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako