• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Feb- 3 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-03 19:56:23

    Watu 246 wamefariki dunia kutokana na mafuriko Zimbabwe

    Watu 246 wamefariki dunia na wengine zaidi ya elfu mbili wameachwa bila nyumba baada ya mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko makubwa nchini Zimbabwe.

    Waziri wa serikali za mitaa, kazi na nyumba wa Zimbabwe Bw Saviour Kasukuwere ameomba msaada toka kwa jumuiya ya kimataifa, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuwasaidia watu walioathiriwa.

    Toka msimu huu uanze Zimbabwe imekuwa na mvua nyingi kuliko kawaida, na kufanya asilimia 85 ya mabwawa ya nchi hiyo kufurika. Waziri Kasukuwere amesema nyumba 2,579, shule 74 na vituo vitano vya afya vimeharibiwa na mafuriko.

    Waziri wa Mazingira, maji na mabadiliko ya hali ya hewa Oppah Muchinguri amesema dola milioni 12 zinahitajika kukarabati mabwawa na mifumo ya usambazaji wa maji iliyoharibiwa.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako