Kwanini manyoya ya panda ni meusi na meupe tu? Hili ni swali gumu kwa watafiti wa biolojia.
Watafiti wa Marekani hivi karibuni wamejibu swali hilo, kwamba rangi mbili zinawasaidia panda kujificha na kufanya mawasiliano.
Watafiti wa tawi la Long Beach la Chuo Kikuu cha California wametawanya manyoya ya panda katika maeneo mbalimbali, na kuyalinganisha na manyoya ya wanyama wa aina 195 wanaokula nyama wakiwemo mbwa, paka na dubu wa aina 39, ili kutafuta uhusiano kati yao na kuthibitisha rangi hizi zinafanya kazi gani.
Watafiti wamegundua kuwa manyoya ya usoni, shingoni, tumboni na kwenye makalio ya panda ni meupe ambayo yanawasaidia kujificha katika mahali penye theluji, na manyoya ya miguuni ni meusi, ambayo yanawasaidia kujifika kwenye kivuli.
Watafiti wamesema panda wana uwezo mdogo wa kumeng'enya chakula, wanaweza kula mianzi tu, na hawaingii kwenye hali ya ubwete katika majira ya baridi kama dubu wengine wanavyofanya, wanatembea mwaka mzima katika sehemu mbalimbali zikiwemo milima inayofunikwa na theluji na misitu ya ukanda wa tropiki.
Lakini rangi maalum usoni mwa panda haziwasaidii kujificha, bali zinawasaidia kuwatambua panda wengine, au kuwaonya washindani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |