Watu wengi wanaogopa buibui, na hata katika baadhi ya vitabu na filamu, buibui wamesimuliwa kama ni shetani. Lakini ukweli ni kwamba buibui ni kiumbe muhimu sana wa kuweka uwiano wa mazingira ya viumbe duniani.
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Basel, Uswisi na Chuo Kikuu cha Lund, Sweden wamehesabu kiasi cha wadudu waliowindwa na buibui duniani kwa mara ya kwanza.
Ripoti ya utafiti waliyoitoa inaonesha kuwa hivi sasa kuna tani milioni 25 za buibui duniani, na kila mwaka buibui hao wanaweza kula tani milioni 400 hadi milioni 800 za chakula. Wadudu wa aina mbalimbali wanachukua asilimia 90 ya chakula chao, na chakula kingine cha buibui ni pamoja na vyura, mijusi, nyoka, samaki, ndege, popo na mimea.
Hivyo watafiti wanaona kuwa buibui wanasaidia kupunguza idadi ya wadudu duniani, na wanatoa mchango mkubwa katika kuhakikisha uwiano kwenye mazingira ya kivumbe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |