• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huenda vikawepo Viumbe kwenye satilaiti ya Enceladus ya sayari ya Saturn

    (GMT+08:00) 2017-04-19 09:17:56

    Shirika la anga ya juu la Marekani limetangaza kuwa limepata ushahidi mpya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa viumbe kwenye satilaiti ya Enceladus ya sayari ya Saturn na satilaiti ya Europa ya sayari ya Jupiter. Watafiti wamesema satilaiti ya Enceladus karibu ina mahitaji yote ya maisha ya viumbe.

    Data zilizotolewa na chombo cha uchunguzi wa sayari ya Saturn cha Cassini zinaonesha, chembe nyingi za Hydrogen ziko kwenye mvuke uliotolewa chini ya bahari iliyofunikwa na barafu kwenye satilaiti ya Enceladus. Watafiti wamekadiria kuwa chembe hizi zinatokana na maji ya baharini yaliyopashwa moto na kiini cha satilaiti hiyo. Na methane ambayo ni kemikali muhimu kwa kutokea kwa viumbe huenda pia inakuwepo baharini.

    Mtafiti mmoja Bw. Hunter Waite alisema, "Ingawa hatuwezi kuchunguza kama viumbe vinakuwepo au la kwenye satilaiti hiyo, lakini tumegundua chemichemi ya nishati kwa maisha ya viumbe. Satilaiti hii inafanana na duka la pipi kwa vijidudu."

    Zamani wanasayansi waliwahi kugundua chemichemi ya maji ya moto chini ya bahari kwenye dunia yetu ambazo zinafanana na zile kwenye satilaiti Enceladus, na chemichemi hizi huwa ni makazii ya viumbe vingi vinavyoishi kwenye bahari yenye kina kirefu. Wakati maji baridi yanapochanganywa na lava ya moto, yanatoa hewa ya Hydrogen, na mabadiliko hayo ya kikemikali yanawapatia viumbe vidogovidogo nishati na lishe. Wataalamu wanaona chanzo cha viumbe vya dunia yetu huenda kilikuwa katika chemichemi hizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako