Shirika la wadukuzi Shadow Brokers wiki iliyopita lilisema kwenye tovuti za SNS kuwa Idara ya usalama ya Marekani NSA iliwahi kuingia kwenye mfumo wa mabenki ya kimataifa, ili kuchunguza maingiliano ya fedha kati ya mabenki ya Mashariki ya Kati na Latin Amerika.
Nyaraka zilizotolewa na shirika hilo zinaonesha kuwa NSA iliwahi kuingia kwenye seva ya Shirika la mawasiliano ya kifedha kati ya mabenki duniani SWIFT, na kudhibiti data za shirika hilo.
Kila siku mabenki na idara za hisa zaidi ya elfu 10 kutoka nchi na sehemu 200 duniani zikitumia mfumo wa SWIFT zinafanya biashara ya matrilioni ya dola za kimarekani.
Shirika hilo limesema litatoa taarifa za kiusalama kwa wakati, na kuwaarifu wateja kukabiliana na vitisho vinavyojulikana, hivi sasa hakuna ushahidi unaoonesha kuwa mfumo huo uliwahi kuingiliwa bila ya idhini.
Lakini baadhi ya vyombo vya habari vinasema mfumo huo uliwahi kuingiliwa na wadukuzi mwaka jana. Mwezi Februari mwaka jana akaunti ya benki kuu ya Bangladesh kwenye benki ya hazina ya Marekani mjini New York ilishambuliwa na wadukuzi kupitia mfumo huo, na kusababisha hasara ya dola za kimarekani milioni 81.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |