Watafiti wa Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani wametoa ripoti kwenye gazeti la Scientific Reports la Uingereza wakisema utafiti wa jeni unaonesha kuwa mamalia wa zama za kale walikuwa na uwezo mkubwa wa kuona wakati wa usiku.
Mabaki ya kihistoria yanaonesha kuwa mamalia wa zama za kale walikuwa na uwezo mkubwa wa kusikia na kuhisi harufu, ambao bado upo kwenye mamalia wa siku hizi. Watafiti wametafiti jeni zinazohusiana na uwezo wa kuona, na kuthibitisha kuwa mamalia wa zama za kale pia wana uwezo mkubwa wa kuona wakati wa usiku.
Mamalia na watambaazi wana vizazi vya pamoja. Mamalia wa kwanza walitokea duniani katika miaka milioni 200 iliyopita. Watafiti walikisia kwamba vizazi vya pamoja vya mamalia na watambaazi havikuwa na uwezo mkubwa wa kuona wakati wa usiku, walizoea kutembea mchana. Baada ya wanyama hao kugawanyika kuwa mamalia na watambaazi, mamalia walipata uwezo mkubwa zaidi wa kuona wakati wa usiku, walilala mchana na kkutoka wakati usiku ili kuepusha kuliwa na watambaazi. Ushindani wa maisha kati ya mamalia na wataambaazi wakiwemo mijusi na nyoka uliwalazimisha mamalia wawe na uwezo mkubwa zaidi wa kutembea gizani.
Mtaalamu wa biolojia wa Chuo Kikuu cha Stanford Prof. Liz Harding alisema uwezo wa kuona mchana au usiku unaonekana ni jambo rahisi, lakini mabadiliko ya jeni husika yanatokana na chaguo la kimaumbile.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |