Wataifit wa Demark na Australia wametafiti nyangumi wachanga wanane aina ya Humpback na mama wawili katika ghuba ya Exmouth magharibi mwa Australia, wamerekodi sauti zao ndogo na kugundua kuwa nyangumi wachanga na mama zao wanaongea kwa sauti ndogo sana ili kuepusha wawindaji.
Mwandishi mkuu wa ripoti ya utafiti Bibi. Simone Videsen alisema nyangumi hao hawataki mazungumzo yao kusikilizwa na maadui. Kwa mfano, nyangumi waauji huenda wakasikiliza sauti zao, na kuthibitisha mahali walipo nyangumi wachanga, halafu kuwasaka.
Bibi Videsen aliongeza kuwa sauti kati ya nyangumi wachanga na mama zao ni ndogo zaidi kuliko sauti za kawaida za nyangumi wakubwa, na ni ndogo kuliko mlio wa nyangumi dume kwa dB 40.
Nyangumi wa Humpback wanajulikana kwa kutoa mlio mkubwa ili kuwaita wenzao, na nyangumi dume hutoa mlio mkubwa ili kuwavutia jike. Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kuona nyangumi hao kuwasiliana kwa sauti ndogo. Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la Functional Ecology la Uingereza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |