Ripoti ya hali ya mimea duniani iliyotolewa na bustani ya mimea ya kifalme ya Uingereza inasema wanasayansi wamegundua aina mpya 1730 za mimea katika mwaka mmoja uliopita, ambazo nyingi zinaweza kutumiwa kuwa chakula au mitishamba.
Hii ni mara ya pili kwa bustani hiyo kutoa ripoti ya mwaka, ambayo ilitolewa na wanasayansi 128 kutoka nchi 12. Ripoti inasema wanasayansi wamegundua aina mpya 5 za muhogo nchini Brazil, ambazo zinafaa kukuzwa na kuwa nafaka inayoweza kukinga ukame na virusi vya mimea. Wanasayansi pia wamegundua aina 9 za mimea ya jenasi ya Mucuna, ambazo zinaweza kutumiwa kuwa mitishamba.
Watafiti wametafiti athari ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa mimea, na kugundua kuwa mimea ambayo ina majani na ngozi nene, inatumia maji kwa ufanisi mkubwa zaidi, na ina mizizi mirefu na migumu zaidi udongoni, ina uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na mabalidiko ya hali ya hewa, kwa sababu sifa hizi za kipekee zinaisaidia kuongeza uwezo wa kuishi na kukabiliana na ukame.
Ripoti hiyo pia imefuatilia tatizo la wadudu na magonjwa ya mimea. Inakadiriwa kuwa kama tatizo la wadudu na vijidudu halitatatuliwa, kilimo cha dunia nzima huenda kitapata hasara kubwa, kwa sababu kutokana na utandawazi duniani, biashara na safari za kimataifa zimeongezeka, na kuongeza uwezekano wa kuenea kwa wadudu na vijidudu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |