Watafiti wa taasisi ya mazingira ya Uholanzi wameonya kwenye gazeti la mabadiliko ya hali ya hewa kuwa kutokana na kuongezeka kwa joto duniani na matumizi ya nishati mijini, joto katika baadhi ya miji duniani huenda likaongezeka kwa nyuzi 8 ifikapo mwaka 2100, hali hii itaathiri vibaya afya za watu, na kuleta shinikizo kubwa kwa matumizi ya maji.
Utafiti huo unasema utoaji wa hewa inayosababisha ongezeko la joto ukiendelea kuongezeka, ifikapo mwishoni mwa karne hii, joto katika miji yenye idadi kubwa ya watu litaongezeka kwa nyuzi 7, na joto katika asilimia 5 ya miji yenye idadi kubwa zaidi litaongezeka kwa zaidi ya nyuzi 8. Kutokana na athari ya ongezeko la joto, mwaka 2050 kwa wastani miji itapata hasara ya kiuchumi ambayo itachukua asilimia 1.4 hadi 1.7 ya pato la taifa la nchini (GNP), , kiasi hiki kitafikia asilimia 2.3 hadi 5.6 ifikapo mwaka 2010, na katika miji yenye hali mbaya zaidi, kiasi hiki huenda kitafikia asilimia 10.9.
Wataifti wamesema joto la mijini huwa ni kubwa zaidi kuliko vijijini, hali hii inaitwa "urban heat island". Watafiti wamependekeza watu kupanda miti mingi zaidi mijini, kujenga mapaa na barabara zinazosaidia kupunguza joto ili kudhibiti ongezeko la joto.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |