Kikundi cha utafiti cha kimataifa kinachoundwa na watafiti wa Ujerumani na Morocco kimetoa ripoti kwenye gazeti la Sayansi la Uingereza ikisema mabaki ya binadamu aina ya Homo Sapiens yana historia ya miaka laki 3 hadi 3.5, ambayo ni ndefu zaidi kuliko historia ya mabaki yaliyogunduliwa zamani kwa miaka laki 1.
Jenasi ya Homo ina aina mbalimbali zikiwemo Habilis, Erectus, Rudolfensis, Gautengensis, Ergaster, Antecessor, n.k. Na binadamu wa kisasa wote ni aina ya Sapien. Watafiti hawajawahi kuthibitisha Homo Sapiens walitokea lini na katika mahali gani. Kabla ya hapo, mabaki ya kale zaidi ya Homo Sapien ni yale yaliyogunduliwa katika Mashariki ya Kati yenye historia ya miaka laki 2, hivyo watafiti wengi walikubali kuwa chanzo cha binadamu kiko Afrika Mashariki.
Watafiti wa Ujerumani na Morocco wamechambua mabaki mapya ya Homo Sapiens yaliyogunduliwa nchini Morocco, na kugundua kuwa mabaki hayo yalitoka kwa zaidi ya binadamu watano. Sura zao na ukubwa wa ubongo wao zinafanana sana na binadamu wa kisasa, lakini mifupa ya vichwa vyao ni mipana na mirefu zaidi. Mtafiti kutoka Taasisi ya mabadiliko ya binadamu ya Max Planck Bw. Jean-Jacques Hublin alisema utafiti unaonesha kuwa Homo Sapiens walikuwa wametapakaa barani Afrika katika miaka laki 3 iliyopita kabla ya kwenda nje ya bara hilo.
Ripoti nyingine iliyotolewa kwenye gazeti hilo inasema mawe ya kiberiti yaliyochimbwa katika eneo hilo nchini Morocco pia yana historia ya miaka laki 3 hadi 3.5, ambayo yanasaidia kuthibitisha historia ya mabaki ya binadamu wa kale.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |