Korea Kaskazini yaendelea kurusha makombora
Korea Kaskazini imejaribu kombora la silaha zake za nyuklia kutoka Pwani ya nchi hiyo. Korea Kaskazini imeendelea na majaribio yake licha ya kuonywa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani.
Wizara ya Ulinzi ya nchi ya Korea Kusini imethibitisha kutekelezwa kwa jaribio hilo.
Korea Kaskazini imeendeleza majaribio haya licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Hivi karibuni Marekani iliionya Korea Kaskazini kuendelea kutekeleza mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.
Hata hivyo Korea Kaskazini imeapa kuendelea na mpango wake huo ikibaini kwamba ni kwa minajili ya usalam wake wa ndani, ikifutilia mbali madai ya Marekani kuwa mpango wake huo unalenga kuhatarisha usalam wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |