• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali isiyo na mvuto yasababisha baadhi ya vijidudu viwe na uwezo mkubwa zaidi wa kuishi

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:16:32

    Utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa Marekani unaonesha kuwa hali isiyo na mvuto katika anga ya juu huenda ikavifanya vijidudu aina ya E. coli viweo na uwezo mkubwa zaidi wa kuishi, tena hali hiyo inaweza kurithiwa na vizazi vingi vijavyo. Habari hii huenda ikawa mbaya kwa safari ya anga ya juu.

    Gazeti la New Scientist la Uingereza limesema watafiti wa Chuo Kikuu cha Houston cha Marekani wamefanya majaribio ya kuweka vijidudu aina ya E. coli kwenye hali isiyo na mvuto. Baada ya vijidudu hao kuzaliana kwa vizazi 1000, vimekuwa na mabadiliko 16 kwenye jeni zao. Baadhi ya mabadiliko yanavisaidia viwe na uwezo mkubwa zaidi wa kukusanyika pamoja na kuunda utando.

    Watafiti wameviweka pamoja vijidudu vilivyobadilika na vijidudu vya kawaida, na kugundua kuwa vijidudu vilivyobadilika vina uwezo mkubwa wa kushindana, vimeunda makundi mengi zaidi kuliko vijidudu vya kawaida kwa mara tatu zaidi. Baada ya kuondoka kwenye hali isiyo na mvuto, vijidudu vilivyobadilika viliendelea kuzaliana, na kizazi cha 30 bado kina uwezo mkubwa wa kushindana. Hii inamaanisha kuwa hali hiyo inaweza kurithiwa.

    Jambo baya ni kwamba kama vijidudu vingine hatari wakiwemo Salmonella vitabadilika na kuwa hatari zaidi kwenye anga ya juu, wanaanga huenda wakakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa. Lakini habari njema ni kwamba dawa za antibiotiki bado zinafanya kazi katika kutibu maabukizi ya vijidudu hivi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako