Watafiti wa Chuo Kikuu cha Miami cha Marekani wamegundua mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka laki 1.3 iliyopita katika Mashariki ya Kati kwa kuchambua mawe ya chokaa pangoni nchini Iran, na kukadiria kuwa hali ya hewa ya Mashariki ya Kati haitakuwa ya unyevu ndani ya miaka elfu 10, hata mvua huenda zitaendelea kupungua katika kanda hiyo kutokana na athari ya mzingo wa dunia kwa kiasi cha mwanga wa jua unaopatikana katika sehemu ya kaskazini ya dunia,.
Mawe ya chokaa mapangoni yanaundwa na Calcium Carbonate ya majini. Kama mazingira yanafaa, kemikali kwenye mawe hayo zinaweza kuonesha mabadiliko ya hali ya hewa katika kanda fulani.
Baada ya kuchambua mawe ya chokaa yanayorekodi mabadiliko ya hali ya hewa ya miaka laki 1 iliyopita katika pango moja kaskazini mwa Iran, watafiti wamegundua kuwa kiasi cha tufani kwenye bahari ya Mediterranean kinahusiana na kiasi cha mwanga wa jua unaopatikana kwenye kanda hiyo. Wakati kiasi cha mwanga wa jua kinapoongezeka, tufani zitaleta mvua nyingi zaidi katika Mashariki ya Kati. Na jambo linaloathiri kiasi cha mwanga wa jua ni mabadiliko ya mzingo wa dunia, na mzingo wa dunia umeamua hali ya hewa ya kanda hiyo iwe ya unyevu katika miaka elfu 10 ijayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |